Jumatatu, 17 Juni 2013

NEW DAY AFRICA FOUNDATION KUFANYA MAAFALI YA KWANZA SIKU YA JUMAMOSI

Siku ya jana ya Jumamosi  kulikuwa na maafali ya kwanza  ya wanafunzi waliokuwa wanahitimu mafunzo ya ushonaji katika  chuo cha NEW DAY AFRICA FOUNDATION  kilichopo Tegeta Kibaoni jijini  Dar es salaam. Chuo kipo chini ya Mkurugenzi Bi. Upendo Kilahiro na Bw. Amon Kilahiro.

Maono ya kuanzisha NE DAY AFRICA FOUNDATION yalianza mwaka 2011 na mwaka 2013 ndipo maono haya yakazaa matunda. Upendo Kilahiro alimshukuru Mungu kwa kutimiza ndoto zake za kuwa na kitu ambacho kinaweza kusaidia jamii kiuchumi.
Kuna vitu ambavyo Mungu amegawa kwa kila mtu lakini wapo wengine wamependelewa kuwa na moyo wa upendo, Bi Upendo kilahiro ni mmojawapo wa kuwa na zawadi ya upendo  kama jina lake linavyoitwa “UPENDO”.

Bi. Upendo na mume wake Amon Kilahiro wamekuwa wakitoa mafundisho hayo ya ushonaji bure na bila ya malipo yoyote. Wanafunzi wamekuwa wakitumia vyerehani vyao bila ya malipo yoyote, gharama za uendeshaji kama umeme unaotumiaka kuendesha mashine za ushonaji zimekuwa zikitolewa  Wakurugenzi hao (Upendo Kilahiro na mume wake). Kwakweli huu ni upendo wa hali ya juu ambao unahitaji kuigwa na watu wote, kwani unaweza kufikiria jinsi maisha ya sasa yalivyoo magumu, lakini watu hawa hawakuweza kuliangalia hilo bali waliangali sana kusaidia wale wenye uhitaji wa kusoma na hawana pesa za kulipia mafundisho yao.
Wahitimu walimshukuru sana Mungu kwa kuwapa mama na baba ambao ni Upendo Kilahiro na mumwe wake Amon Kilahiro kuwafungua katika giza na kuwaweka katika nuru ya mafanikio ya kimaisha. Elimu waliyopata sio elimu ya theory bali ni elimu ya vitendo.

Wahitimu walionekana kuwa na sura za huruma wakati kumuaga Upendo Kilahiro na mwalimu wao  kwani walisema wanatamani kuwa naye siku zote , na hii ni kwasababu ya upendo waliokuwa nao wakati wapo masomoni na wengine walioneka kutokwa na machozi. 
Kuna baadhi ya wanafunzi waliweza kupita mbele na kueleza kile ambacho wamekipata chuoni. Baadhi yao walisema wao walifika pale chuoni wakiwa hawajui hata kuchomeka sindano katika mashine ya kushonea, ila baada ya kufundishwa na mwalimu wao waliweza kujua kuchomeka sindano na kuweza kushona nguo za aina yoyote. Wahitimu hao walisema kwa sasa wanaweza kushona mshono wowote.

Wahitimu hao waliweza kuimba wimbo wa kumuaga Upendo Kilahiro,  mwalimu wao na uongozi mzima wa chuo hicho. Wimbo ulikuwa umejaa majonzi  kutokana yale waliotendewa wanahitimu hao wakiwa masomo.Walisema wamejifunza mambo mengi ya kimwili na kiroho na kubwa zaidi wamejipatia ujuzi wa ushonaji.


Mbali ya hayo yote, Mkurugenzi Upendo Kilahiro alimshukuru sana Mungu kwa kutimiza ndoto yake aliyokuwa nayo kwa muda mrefu ya kuweza kusaidia jamii. Kwake anasema ni mmoja wa muujiza mkubwa Mungu amefanya katika maisha yake. Upendo alionekana kuongea kwa hisia kali sana juu ya mafanikio aliyokuwa nayo. Amesema mara nyingi amekuwa busy sana na kazi za kifamili, kihuduma katika kazi ya Mungu, safari mbalimbali nje ya Tanzania kama UK na Canada kwa kazi ya Mungu na
wakati huo huo anatakiwa kutimiza ndoto yake ya kuisadia jamii hasa suala hili la wanafunzi wa ushonaji. Amekuwa akijibana kwa mambo mengi hasa katika suala la pesa ili kuhakikisha hawa wanafunzi wanapata mahitaji yote ya msingi katika suala lao la ushonaji. Wanafunzi waliweza kuvaa sale zao ambazo wamezitengeza wenyewe na liliwemo vazi alilo vaa Upendo Kilahiro. Wanafunzi hawa ukiangalia mavazi hao, kwa kweli utasema ni wabunifu wa hali ya juu sana.

UPENNDO KILAHIRO alisema anajisikia kuwa mpweke sana kwa kuangana na wanafunzi hawa kwani amekuwa akiishi nao kama familia na sio kama wanafunzi. Ila alisema kila jambo lina mwanzo na mwisho kwahiyo hata hawa wanafunzi wake umefika wakati wa kuondoka. aliwaomba wanafunzi wazidi kufika chuoni hapa kama kuna jambo watakuwa wanahitaji kutoka kwake, milango iko wazi na yeye atawasaidia bila ya kujali kuwa wamemaliza masomo yao.

Alisema lengo lake ni kuona hawa viajana wanapata kazi zao za kujitegemea ili waweze kuwa mchango mkubwa katika Taifa la Tanzania kwani bado wana nguvu za kulitumikia Taifa lao. Watu kama hawa ambao walikuwa hawana ujuzi wako wengi sana mitaani wanashindwa watu wa kuwainua ili wasimame wenyewe, alisema.

-------------------------------------

Katika hotuba yake, alikuwa na haya machace ya kusema:

NEW  DAY AFRICA FOUNDATION (NEDAFO)

NEW  DAY AFRICA FOUNDATION (NEDAFO)  ni shirika la Kikristo linatoa huduma za kiroho na za kijamii. Shirika hili lilianza rasmi mwaka 2011 chini ya mbeba maon Bi. Upendo Kilahiro na daadae shirika hili lilipanuka na kuongeza kwa kusaidiwa na mumewe Bw. Amon Kilahiro hadi kupata uongozi wa

NEDAFO.

Shirika hili lilianza hapa Tanzania lakini lina maono ya kusambaa mataifa yote ya Afrika kwa lengo la kuwapa elimu na tumaini jipya kwa kila mmoja hasa wanawake, wasichana na watoto.Shirika hili lilianza miaka mitatu iliyopita lakini mwaka huu 2013 tumeanza kutoa huduma za kijamii. NEDAFO imeweza kutoa mafunzo ya ushonaji kwa wanawake na wasichana, nah ii ni sehemu tu ya mengi  ambayo NEDAFO inamtumainia Mungu kutuwezesha kuyafanya katika siku za usoni ili kufikia lengo la maono tuliyonayo.

Shirika hili limekuwa likiwafundisha wanafunzi bure na Mkurugenzi amekuwa akiwajibika kuhakikisha wanafunzi wanapata elimu bora, vitendea kazi vya kisasa vinakuwepo, ma pia kuhakikisha wanafunzi wanakuwa katika maadili yale Mungu anahitaji kwa kila mwanadamu kuwa nayo.

UTENDAJI
NEDAFO inafanya kazi ya kuwaendeleza wale wenye uhitaji wa kujiendeleza ili waweze kujikimu katika maisha, kujisimamia kujiajiri na kuweza kuwasaidia wengine kwa yale waliojifunza katika shirika hili la NEDAFO

WASILIANA NASI KWA SIMU
+255 757 578114
www.upendokilahiro.blogspot.com



MUNGU AKUBARIKI


TUONE YALIYOTOKEA
 Mkurugenzi wa New Day Africa Foundation, Bi. Upendo Kilahiro

Upendo Kilahiro
 Mkurugenzi wa New Day Africa Foundation, Bi. Upendo Kilahiro akiwa na baba yake ambaye alikuwa mgawaji wa vyeti siku hii
Mkurugenzi wa New Day Africa Foundation, Bi. Upendo Kilahiro akiwa na furaha ya ajabu kutimiza ndoto yake, Vazi alilovaa limebuniwa na wanafunzi wake.
 Mkurugenzi wa New Day Africa Foundation, Bi. Upendo Kilahiro akimshukuru Mungu kwa kumuwezesha kufika pale alipokuwa akiota kila siku kupafikia.
 Hapa ni nyumbani kwa Upendo Kilahiro Tegeta Kibaoni
 Mpambaji akiwa kazini kuhakikisha mambo yanakwenda sawa.
 ..mmoja wa viongozi wa juu katika New Day Africa Foundation akiwa na furaha ya ajabu
 Wa pili kutoka kulia na mama na Upendo Kilahilo na anayefuatia ni baba na upendo Kilahilo wakiwa katika picha ya pamoja.

 Wahitimu wa chuo cha NEW  DAY AFRICA FOUNDATION (NEDAFO) wakiwa katika picha ya pamoja.
 Mavazi haya waliyovaa hawa wahitimu yamebuniwa na wao wenyewe.

 Huu ni uongozi wa NEW  DAY AFRICA FOUNDATION (NEDAFO)

Wahitimu wakiwa wamejiaandaa kupokea vyeti vya kuhitimu
 Wahitimu wakionyesha mishono ya mavazi yao waliyoibuni wakiwa chuoni







 Kulia ni mtoto wa Upendo Kilahiro ambaye naye amejifunza kushona nguo kwa kutumia mashine za kisasa zilizopo hapo chuoni. Hapa akionekana akisali wakati wa kuombea chakula na vinjwaji
 Wahitimu wakiwa katika sala ya kuombea vinywaji na chakula

 Mkurungenzi wa NEW DAY AFRICA FOUNDATION, Upendo Kilahiro akijitambulisha
 Mwalimu wa NEW DAY AFRICA FOUNDATION akijitambulisha

 Mkurugenzi wa NEW DAY AFRICA FOUNDATION Upendo Kilahiro akiongea na wahitimu

 Mkurugenzi wa NEW DAY AFRICA FOUNDATION akiita majina ya wahitimu kuchukua vyeti vyao vya kumaliza mafunzo ya ushonaji.










 Wahitimu wakionysha vyeti vya vya ushindi kumaliza masomo yao ya ushonaji.


 Mwalimu akiwa na wahitimu wakiimba wimbo wa kuagana na uongozi mzima wa NEW DAY AFRICA FOUNDATION




Mpiga Picha
Rumafrica
www.rumafrica.blogspot.com

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni